Katika sehemu hii ya Kozi za Utalii, utapata matangazo na taarifa za vyuo na taasisi mbalimbali zinazotoa mafunzo ya utalii kwa ngazi ya cheti (Certificate) na stashahada (Diploma). Kozi hizi zinahusisha fani kama usimamizi wa utalii, uhifadhi wa maliasili, uongozaji wa watalii, huduma za hoteli na malazi, mapokezi (front office), usafiri na usimamizi wa safari, pamoja na masoko ya utalii. Mafunzo haya yanalenga kuwajengea wanafunzi ujuzi wa vitendo na maarifa ya kitaaluma ili kutoa huduma bora kwa wageni wa ndani na wa kimataifa, kulinda rasilimali za utalii, na kuchangia ukuaji wa sekta ya utalii nchini Tanzania. Katika category hii utaona maelezo kuhusu sifa za kujiunga, muda wa masomo, ada, ratiba, mafunzo kwa vitendo (field na practical), pamoja na vyeti vinavyotolewa baada ya kuhitimu. Sehemu hii inawafaa wahitimu wa sekondari, vijana wanaopenda utalii, na watu wanaotaka kupata ajira katika hoteli, hifadhi za taifa, makampuni ya utalii, au kujiajiri katika shughuli za utalii.
We could not find any results for your search...
Following tips might help you to get better results
Use more general keywords
Check spelling of position
Reduce filters, use less of them
