NAANZAJE BIASHARA YA NAFAKA?
Moja ya Biashara ni nzuri kufanya, Hii sio biashara ya msimu, ni biashara ya mwaka mzima kutokana na uhitaji wake wa kila siku.
Anza kwa kuandaa mchanganuo mfupi wa biashara ya Duka la kuuza Mazao ya Nafaka.
Andika mahitaji ya muhimu unayotakiwa kuwa nayo kuuza Nafaka na mazao ya kilimo mfano alizeti, soya, unga, mahindi, Mchele, Sukari, karanga,mafuta ya kula nk.
Pia tambua uleunga kuwauzia wateja aina gani
MTAJI.
Utapata mtaji fedha kununua
Nafaka pamoja na
gharama zingine kama kukodi eneo la Biashara, usafiri nk.
Makadirio ya mtaji ni kuanzia 5M kwa mjini, lakini mtaji unaweza kuomba kulingana na mahali.
Kabla ya kununua vitu ni muhimu kufanya utafiti unaohitajika usije kuleta maharage mengi kumbe eneo la unga zaidi na wana mboga zao za majani.
Tafuta ENEO lenye mali mkubwa wa watukama maeneo ya makazi, center na kwenye masoko.
Nafaka utanunua kwa wakulima au kwamawakala wakubwa wanaouza Mazao ya nafaka kwa bei ndogo.
Kama huna mtaji mkubwa unaweza anza kuongeza thamani nafaka, mfano kuweka kwenye package nzuri za kilo 1,2 5,10 na kuuza. Unaweza kuweka nembo pia.
Biashara hii pia ni nzuri kwa waajiriwa kwani nafaka ni vitu vivyohesabika hivyo unaweza kufatilia mauzo.
Pia unaweza kuwa dalali wa mazao. Kama uko vijijini au sehemu ya mazao unatafuta wateja unawapelekea Kwa wakulima au unachukua mzigo kwa wakulima ukipata mteja.
Comments