BIASHARA YA KARANGA ZA MAYAI
Mahitaji
Karanga 1kg
Mayai 2/3 itategemeana na ukubwa wa mayai
Sukari vijiko 6 vya chakula
Unga wa ngano robo kilo
Chumvi kijiko 1 cha chakula
Vanilla au hiliki (inasaidia kuzipa harufu nzuri karanga zako)
Mafuta ya kukaanga lita 1
Jinsi ya kuandaa
Gonga mayai koroga kwenye kikombe
Mimina sukari, chumvi, vanilla kisha endelea kukoroga mpaka mchanganyiko uwe mzuri
Weka karanga kwenye chombo
Miminia mchanganyiko wa mayai na sukari kwenye karanga
Koroga mpaka zichanganyike vizuri
Weka unga wa ngano kidogo kidogo uuku unakoroga.
Ukishakuwa mkavu fanya kuupepeta ili ziachane ziwe karanga moja moja
Weka mafuta jikoni
Moto usiwe mkali sana.
Mafuta yakishapata moto kiasi weka karanga.
Zingatia kugeuza mara kwa mara ili zisiungue.
Zikishabadilika rangi kidogo kuwa kahawia zitoe.
Zichuje mafuta, ziache zipoe.
Hapo tayari kwa kuliwa.
USHARI KWA MFANYABIASHARA
Usafi wakati wa maandalizi ya upishi wa karanga.
Chambua karanga vizuri toa uchafu wote.
Usiache karanga zikaungua zitakuwa chungu sana
Vipimo: wakati wa kufungasha karanga kuwa makini hakikisha unapima vizuri ili upate faida na wateja wako waridhike pia.
Tafuta soko la biashara yako madukani, mtaani, mashuleni, sokoni.
Tafuta wateja popote unapokuwa, tembea na bidhaa zako
Comments